Staff

Sharaja Ya Radio Jangwani

WASICHANA kutoka Kaunti ya Marsabit wako na kila sababu ya kutabasamu baada ya aliyekuwa Miss Tourism 2013 kaunti ya Marsabit Bi Qabale Duba kutoa vitambaa vya kuzuia hedhi ama sodo kwa mpango mzima almarufu PAPA Project, Bi Qabale alisema kuwa hatua hiyo inatarajiwa kutoa suluhu kwa wasichana wengi ambao hukosa kuhudhuria masomo wakati wanapohudhuria hedhi kutokana na ukosefu wa sodo.

Bi Qabale pia alitaja maswala ya ukeketaji kuwa ni kinyume cha sheria na ni lazima kamwe usitendwe katika kaunti ya marsabit, Pia ni kinyume cha sheria kumsaidia mtu yeyote kufanya ukeketaji wa namna yoyote.

Qabale alisisitiza kuwa Wasichana wengi wamefariki kutokana na kupoteza damu au kwa ugonjwa wa kuambukizwa kutokana na utaratibu huu. Na kwa kina dada waliokeketwa wanaweza pia kupata matatizo wakati wa uzazi. Mkutano huo ulihudhuriwa na waakilishi wa vikundi mbali mbali ya akina kutoka jamii zote kumi na nne katika kaunti ya Marsabit.

Leave A Comment

Your Comment
All comments are held for moderation.